Masharti ya Huduma
Karibu kwenye Facebook!
Facebook hujenga teknolojia na huduma ambazo huwezesha watu kuwasiliana, kujenga jumuiya mbalimbali na kukuza biashara. Masharti haya yanatawala matumizi yako ya Facebook, Messenger na bidhaa, vipengele, programu, huduma, teknolojia na programu nyingine tunazotoa (Bidhaa za Facebook au Bidhaa), isipokuwa pale ambapo tumeeleza moja kwa moja kwamba masharti tofauti (wala sio haya) yanatumika. Bidhaa hizi zinaletwa kwako na kampuni ya Facebook Ireland Limited.
Hatukutozi ada zozote kwa kutumia Facebook au bidhaa na huduma nyingine zilizo chini ya Masharti haya.. Badala yake, biashara na mashirika yanatulipa ili kukuonyesha matangazo ya bidhaa na huduma zao. Kwa kutumia Bidhaa zetu, unakubali kwamba tunaweza kukuonyesha matangazo tunayofikiri yatakufaa na mambo yanayokupendeza. Tunatumia data ya kibinafsi kusaidia kubaini ni matangazo yepi tunakuonyesha.
Hatuuzi data yako ya kibinafsi kwa watangazaji na hatushiriki maelezo ambayo yanakutambulisha moja kwa moja (kama vile jina lako, anwani yako ya barua pepe au maelezo mengine ya anwani) na watangazaji isipokuwa ikiwa utatupa kibali mahususi. Badala yake, watagazaji wanaweza kutuambia mambo kama vile aina ya hadhira ambao wangependa waone matangazo yao na sisi tunaonyesha matangazo hayo kwa watu ambao huenda wakakupendeza. Tunawapa watangazaji ripoti kuhusu utendakazi wa matangazo yao ili kuwasaidia kuelewa jinsi watu wanavyotangamana na maudhui yao. Angalia sehemu ya 2 hapa chini ili ujifunze zaidi.
Sera yetu ya Data inaeleza jinsi tunavyokusanya na kutumia data yako ya kibinafsi ili kubaini baadhi ya matangazo unayoyaona na kutoa huduma nyingine zote zilizofafanuliwa hapa chini. Unaweza pia kuenda kwenye mipangilio wakati wowote ili kukagua chaguo za faragha ulizo nazo kuhusu jinsi tunavyotumia data yako.
1. Huduma tunazotoa
Lengo letu ni kuwawezesha watu kujenga jumuiya na kuileta dunia pamoja. Ili kusaidia kuendeleza lengo hili, tunakutolea Bidhaa na huduma zilizofafanuliwa hapa chini:Tunakutolea tajiriba iliyobinafsishwa:
Tajiriba yako kwenye Facebook sio kama ya mtu mwingine yeyote: kutoka kwa machapisho, hadithi, matukio, matangazo, na maudhui mengine unayoyaona kwenye Taarifa au jukwaa letu la video hadi kwenye Kurasa unazofuata na vipengele vingine unavyoweza kutumia, kama vile Inayovuma, Marketplace, na utafutaji. Tunatumia data tuliyo nayo - kwa mfano, kuhusu miunganisho unayofanya, chaguo na mipangilio unayoteua, na unachoshiriki na kufanya ndani na nje ya Bidhaa zetu - kubinafsisha tajiriba yako. Tunakuunganisha na watu pamoja na mashirika unayoyajali:
Tunakusaidia kutafuta na kuunganisha watu, vikundi, biashara, mashirika, na wengine unaowathamini kwenye Bidhaa za Facebook unazotumia. Tunatumia data tuliyo nayo ili kufanya mapendekezo kwa ajili yako na wengine - kwa mfano, vikundi vya kujiunga, matukio ya kuhudhuria, Kurasa za kufuata au kutuma ujumbe, maonyesho ya kutazama, na watu unaoweza kutaka kuwa marafiki nao. Muingano thabiti inaboresha jumuiya, na tunaamini huduma zetu ni muhimu zaidi wakati watu wameunganishwa na watu, vikundi, na mashirika wanayojali. Kukuwezesha ili kujieleza na kuzungumzia kuhusu mambo muhimu kwako:
Kuna njia nyingi za kujieleza kwenye Facebook na kuwasiliana na marafiki, familia, na wengine kuhusu kile ambacho ni muhimu kwako - kwa mfano, kushiriki visasisho vya hali, picha, video, na hadithi katika Bidhaa za Facebook unazotumia, kutuma ujumbe kwa rafiki au watu kadhaa, kuunda matukio au vikundi, au kuongeza maudhui kwenye wasifu wako. Pia tumezindua, na kuendelea kuchunguza, njia mpya za watu kutumia teknolojia, kama vile ukweli uliojadiliwa na video ya 360 kuunda na kushiriki maudhui ya kujieleza zaidi na kushirikisha kwenye Facebook. Kukusaidia kugundua maudhui, bidhaa, na huduma zinazoweza kukupendeza:
Tunakuonyesha matangazo, ofa, na maudhui mengine yaliyodhaminiwa ili kukusaidia kugundua maudhui, bidhaa, na huduma zinazotolewa na biashara nyingi na mashirika yanayotumia Facebook na bidhaa nyingine za Facebook. Sehemu ya 2 hapa chini inaeleza haya kwa undani zaidi. Kukabiliana na mienendo hatari na kulinda na kuunga mkono jumuiya yetu:
Watu watajenga tu jumuiya kwenye Facebook iwapo watajihisi salama. Tunaajiri timu za kujitolea kote ulimwenguni na kukuza mifumo mahiri ya kiufundi ili kutambua matumizi mabaya ya Bidhaa zetu, mienendo hatari dhidi ya watu wengine, na hali ambazo tunaweza kusaidia kuunga mkono au kulinda jumuiya yetu. Iwapo tutagundua maudhui au maadili kama haya, tutachukua hatua inayofaa - kwa mfano, kutoa msaada, kuondoa maudhui, kuzuia ufikiaji kwa vipengele fulani, kulemaza akaunti, au kuwasiliana na watekelezaji wa sheria. Tunashiriki data kwa Kampuni za Facebook zingine tunapogundua matumizi mabaya au mienendo hatari za mtu anayetumia mojawapo ya Bidhaa zetu. Kutumia na kukuza teknolojia mahiri ili kutoa huduma salama na za utendaji kwa kila mtu:
Tunatumia na kukuza teknolojia mahiri - kama vile ujasusi wa kisasa, mifumo ya mafunzo ya mashine, na ukweli uliojadiliwa - ili watu waweze kutumia Bidhaa zetu kwa usalama bila kujali uwezo wa kimwili au eneo la kijiografia. Kwa mfano, teknolojia kama hii huwasaidia watu walio na matatizo ya kuona, kuelewa nini au nani yuko kwenye picha au video zilizosambzwa kwenye Facebook au Instagram. Pia tunajenga mitandao ya kisasa na teknolojia ya mawasiliano ili kuwasaidia watu zaidi kuungana kwenye mtandao katika maeneo yaliyo na ufikiaji wa kipimo. Na tunakuza mifumo ya kiotomatiki ili kuboresha uwezo wetu wa kutambua na kuondoa shughuli za matusi na hatari ambazo zinaweza kudhuru jumuiya yetu na uadilifu wa Bidhaa zetu Kufanya utafiti wa njia za kuboresha huduma zetu:
Tunajihusisha katika utafiti ili kukuza, kujaribu na kuboresha Bidhaa zetu. Hii inajumuisha uchanganuzi wa data tuliyo nayo kuhusu watumiaji wetu na kuelewa jinsi watu hutumia Bidhaa zetu, kwa mfano, kwa kuendesha utafiti na kujaribu na kutatua vipengele vipya. Sera yetu ya Data inafafanua jinsi tunavyotumia data ili kusaidia utafiti huu kwa madhumuni ya kukuza na kuboresha huduma zetu. Kutoa tajiriba thabiti na nzuri kwenye Bidhaa za Kampuni ya Facebook:
Bidhaa zetu hukusaidia kutafuta na kuungana na watu, vikundi, biashara, mashirika, na nyinginezo ambazo ni muhimu kwako. Tunabuni mifumo yetu ili tajiriba yako iwe thabiti na nzuri kwenye Bidhaa za Kampuni ya Facebook tofauti unazotumia. Kwa mfano, tunatumia data kuhusu watu unaoshirikiana nao kwenye Facebook ili kukurahisishia kuungana nao kwenye Instagram na Messenger, na tunakuwezesha kuwasiliana na biashara unayofuata kwenye Facebook kupitia Messenger. Kuwezesha ufikiaji wa ulimwengu huduma zetu:
Ili kuendesha huduma yetu kiulimwengu, tunahitaji kuhifadhi na kushiriki maudhui na data kwenye vituo na mifumo yetu ya data ulimwenguni kote, ikijumuisha nje ya nchi yako ya makazi. Muundomsingi huu unaweza kuendeshwa au kudhibitiwa na Facebook, Inc., Facebook Ireland Limited, au vyama tanzu vyake. 2. Jinsi huduma zetu hufadhiliwa
Badala ya kulipa ili kutumia Facebook na bidhaa na huduma nyingine tunazotoa, kwa kutumia Bidhaa za Facebook zilizo chini ya Masharti haya, unakubalu kwamba tuaweza kukuonyesha matangazo ambayo biashara na mashirika hutulipa ili tutangaze kwenye na nje ya Bidhaa za Kampuni ya Facebook. Tunatumia data yako ya kibinafsi kama vile maelezo kuhusu shughuli na mambo yanayokuvutia, ili kukuonyesha matangazo ambayo yanakufaa zaidi.
Kulinda faragha ya watu ni kipengele muhimu katika uundaji wa mfumo wetu wa matangazo Hii inamaanishwa kwamba tunaweza kukuonyesha matangazao muhimu na yanayokufaa bila kukutambulisha kwa watangazaji. Hatuuzi data yako ya kibinafsi. Tunaruhusu watangazaji kutuarifu kuhusu mambo kama vile lengo lao kibiashara na aina ya hadhira wanaotaka waone matangazo yao (kwa mfano, watu kati ya umri wa miaka 18-35 ambao wanapenda kuendesha baiskeli). Kisha tunaonyesha tangazo lao kwa watu ambao huenda wakavutiwa.
Pia, tunawapa watangazaji ripoti kuhusu utendakazi wa matangazo yao ili kuwasaidia kuelewa jinsi watu wanavyotangamana na maudhui yao kwenye au nje ya Facebook. Kwa mfano, tunatoa demografia ya kawaida na maelezo yanayopendelewa kwa watangazaji (kwa mfano, kuwa tangazo lilitazamwa na mwanamke kati ya umri wa miaka 25 na 34 anayeishi Madrid na hupenda uhandisi wa programu) ili kumsaidia kuelewa bora zaidi hadhira yake. Hatushiriki maelezo ambayo yanakutambua moja kwa moja (maelezo kama vile, jina lako au anwani yako ya barua pepe ambayo inaweza kutumiwa kuwasiliana nawe au unakutambulisha) isipokuwa ikiwa utatupa kibali mahususi. Jifunze zaidi hapa kuhusu jinsi matangazo ya Facebook hufanya kazi.
Tunakusanya na kutumia data yako ya kibinafsi ili kutoa huduma ulizofafanuliwa hapo juu. Unaweza kujifunza kuhusu jinsi ya kukusanya na kutumia data yako kwenye Sera yetu ya Data. Una udhibiti wa aina ya matangazo na watangazaji unaowaona na aina ya taarifa tunazotumia kubaini ni matangazo yepi tunayokuonyesha. Jifunze zaidi.
3. Juhudi zako kwa Facebook na jumuiya yetu
Tunatoa huduma hizi kwako pamoja na wengine ili kusaidia kuendeleza lengo letu. Kwa kubadilishana, tunakuhitaji ufanye juhudi zifuatazo:1. Ni nani anayeweza kutumia Facebook
Watu wanapounga mkono maoni na vitendo vyao, jumuiya yetu inakuwa salama na inawajibika zaidi. Kwa sababu hii, ni lazima: - Utumie jina lile ambalo unalolitumia katika maisha ya kila siku.
- Utoe maelezo sahihi kujihusu:
- Uunde akaunti moja tu (yako binafsi) na utumie kalenda yako ya matukio kwa malengo ya kibinafsi.
- Usisamabaze nenosiri lako, kutoa ufikiaji kwa wengine kwenye akaunti yako ya Facebook, au kuhamisha akaunti yako kwa mtu mwingine yeyote (bila kibali chako).
- Uko chini ya umri wa miaka 13.
- Wewe ni mkosaji wa ngono uliyehukumiwa.
- Tulilemaza akaunti yako hapo awali kwa ukiukaji wa Masharti na Sera Zetu.
- Umepigwa marufuku kutokana na kupokea bidhaa, huduma, au programu zetu chini ya sheria zinazotumika.
2. Unachoweza kushiriki na kufanya kwenye Facebook
Tunataka watu watumie Facebook kujieleza na kushiriki maudhui ambayo ni muhimu kwao, lakini sio kwa gharama ya usalama na ustawi wa wengine au uadilifu wa jumuiya yetu. Kwa hivyo unakubali kutoshiriki katika mienendo iliyofafanuliwa hapa chini (au kuwezesha au kuwasaidia wengine kufanya hivyo): - Huenda usitumie Bidhaa zetu kufanya au kusambaza chochote:
- Kinachokiuka Masharti haya, Viwango vya Jumuiya na masharti na sera nyingine ambazo zinatumika katika matumizi yako ya Facebook.
- Kinachokiuka sheria, kinachopotosha, kunachobagua au cha ulaghai.
- Kinachoingilia au kukiuka haki za mtu mwingine, zikiwemo haki zake za mali miliki.
- Huenda usiweze kupakia virusi au msimbo hasidi au kufanya jambo lolote ambalo linaweza kulemaza, kuweka mzigo mkubwa, au kuharibu ufanyikazi bora au uonekanaji wa Bidhaa zetu.
- Huenda usifikie au kukusanya data kutoka kwa Bidhaa zetu kwa kutumia njia za kiotomatiki (bila kibali chetu cha mapema) au kujaribu kufikia data ambayo huna kibali cha kufikia.
3. Vibali unavyotupatia
Tunahitaji vibali fulani kutoka kwako ili kutoa huduma zetu: - Kibali cha kutumia maudhui unayounda na kushiriki: Baadhi ya maudhui ambayo unashiriki au kupakia, kama vile picha au video, yanaweza kulindwa kupitia sheria za mali miliki.Una miliki haki za miliki (mambo kama vile haki miliki au alama za biashara) katika maudhui yoyote ambayo unaunda na kushiriki kwenye Facebook na Bidhaa Nyingine za Kampuni ya Facebook unazotumia. Hakuna chochote katika Masharti haya kinachokunyima haki ya kumiliki maudhui yako. Uko huru kushiriki maudhui yako na mtu mwingine yeyote, popote unapotaka.Hata hivyo, ili kutoa huduma zetu, tunakuhitaji utupe vibali fulani kisheria (vinavyojulikana kama (‘leseni’) kutumia maudhui haya. Hii ni kwa lengo pekee la kutoa na kuboresha Bidhaa na huduma zetu kama ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 1 hapo juu.Haswa, unaposhiriki, kuchapisha au kupakia maudhui ambayo yako chini ya haki za mali miliki kwenye au kuhusiana na Bidhaa zetu, unatupa leseni isiyobagua, isiyoweza kuhamishwa, isiyoweza kutolewa kwa watu wengine wa chini, isiyo na mrabaha na ya kimataifa kupanga, kutumia, kusambaza, kubadilisha, kuendesha, kunakili, kuonyesha kwenye umma, kutafsiri na kuunda kazi zalishwa kutokana na maudhui yako (kulingana na mipangilio yako ya faragha na programu. Hii inamaanisha, kwa mfano, kwamba ikiwa utashiriki picha kwenye Facebook, unatupa kibali cha kuhifadhi, kunakili na kuishiriki na watu wengine (tena, kulingana na mipangilio yako) kama vile watoaji huduma wanaotumia huduma zetu au Bidhaa nyingine za Facebook unazotumia. Muda wa matumizi ya leseni hii utakwisha wakati maudhui yako yatafutwa kutoka kwenye mifumo yetu.Unaweza kufuta maudhui moja baada ya nyingine au yote kwa pamoja kwa kufuta akaunti yako. Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kufuta akaunti yako. Unaweza kupakua nakala ya data yako wakati wowote kabla ya kufuta akaunti yako.Unapofuta maudhui, hayataonekana tena kwa watumiaji wengine, ingawa yanaweza kuendelea kuwepo mahali pengine kwenye mifumo yetu ambapo:
- hatua za dharura haziwezi kuchukuliwa kutokana na vizuizi vya kiufundi (katika hali hii, maudhui yako yatafutwa ndani ya siku zisizozidi 90 kuanzia tarehe ulipoyafuta);
- watu wengine wametumia maudhui yako kwa mujibu wa leseni hii na hawajayafuta (katika hali hii, leseni itaendelea kutumika hadi maudhui hayo yatakapofutwa); au
- endapo kufutwa mara moja kunaweza kudhibiti uwezo wetu:
- kuchunguza au kutambua shughuli zilizopigwa marufuku au ukiukaji wa masharti na sera zetu (kwa mfano, kutambua au kuchunguza matumizi mabaya ya Bidhaa au mifumo yetu);
- kufuata wajibu wa kisheria, kama vile utunzaji wa ushahidi; au
- kutii ombi la mamlaka ya mahakama au kiutawala, shirika la kutekeleza sheria au la serikali;
katika hali hii, maudhui yatawekwa kwa muda usiozidi unavyostahili kwa madhumuni yaliyosababisha kuwekwa kwake (kipindi halisi kitakuwa tofauti kwa misingi ya tukio moja hadi lingine). Katika kila hali hapo juu, leseni hii itaendelea kutumika hadi maudhui yafutwe kikamilifu. - Kibali cha kutumia jina , picha ya wasifu, na maelezo yako kuhusu vitendo vyako kwa matangazo na maudhui yaliyodhaminiwa: Unatupatia kibali cha kutumia jina na picha yako ya wasifu na maelezo kuhusu hatua ambazo umezichukua kwenye Facebook karibu na au kuhusiana na matangazo, ofa, na maudhui mengine yanayodhaminiwa tunayoonyesha katika Bidhaa zetu, bila fidia yoyote kwako. Kwa mfano, tunaweza kuonyesha marafiki zako kuwa umependezwa na tukio lililotangazwa au umependezwa na Ukurasa ulioundwa na chapa ambayo imetulipa kuonyesha matangazo yake kwenye Facebook. Matangazo kama haya yanaweza kuonekana tu na watu walio na kibali chako cha kuona hatua ulizochukua kwenye Facebook. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mipangilio na mapendeleo yako ya tangazo.
- Kibali cha kusasisha programu unayotumia au kupakua: Ikiwa utapakua au kutumia programu yetu, unatupa kibali cha kupakua na kusakinisha masasisho ya programu panapopatikana.
4. Mipaka ya kutumia mali miliki yetu
Iwapo unatumia maudhui yanayolindwa na haki za mali miliki ambazo tuko nazo na kuzifanya zipatikane kwenye Bidhaa zetu (kwa mfano, taswira, miundo, video, au sauti tunazotoa unazoongeza kwenye maudhui unayounda au kushiriki kwenye Facebook), tunabakiza haki zote za maudhui hayo (lakini sio yako). Unaweza tu kutumia hakimiliki au alama zetu za biashara (au alama yoyote kama hiyo) kama ilivyoruhishwa moja kwa moja na Miongozo yetu ya Matumizi ya Chapa au kwa kibali chetu kilichoandikwa mapema. Lazima upate kibali chetu kilichoandikwa (au kibali chini ya leseni ya chanzo wazi) ili kurekebisha, kuunda kazi za ubunifu za, kutawanyisha, au vinginevyo kujaribu kuopoa msimbo wa chanzo kutoka kwetu. 4. Masharti ya ziada
1. Kusasisha Masharti yetu
Tunafanya kazi mara kwa mara ili kuimarisha huduma zetu na kukuza vipengele vipya ili kuboresha Bidhaa zetu kwa ajili yako pamoja na jumuiya yetu. Kutokana na hilo, tunaweza kuhitaji kusasisha Masharti haya mara kwa mara ili kuonyesha kwa usahihi huduma na vitendo vyetu. Tutafanya mabadiliko ikiwa tu masharti haya hayafai tena au ikiwa hayajakamilika na ikiwa tu mabadiliko yanafaa na yanazingatia masilahi yako ipasavyo. Tutakuarifu (kwa mfano, kupitia barua pepe au Bidhaa zetu) angalau siku 30 kabla ya sisi kufanyia Masharti haya mabadiliko na kukupa nafasi ya kuyakagua kabla yaanze kutumika, isipokuwa kama mabadiliko hayo yanahitajika kisheria. Pindi tu Masharti yoyote yaliyosasishwa yanatumika, utafungwa nayo iwapo utaendelea kutumia Bidhaa zetu. Tunatumai kuwa utaendelea kutumia Bidhaa zetu, lakini iwapo hukubaliani na Masharti yetu yaliyosasishwa na hutaki tena kuwa mmojawapo wa jumuiya ya Facebook, unaweza kufuta akaunti yako wakati wowote. 2. Usitishaji au ukomeshaji wa akaunti
Tunataka Facebook liwe eneo ambalo watu wanajihisi huru na salama kujieleza na kushiriki mawazo na hoja zao. Ikiwa tutabaini kwamba umekiuka Masharti au Sera zetu kwa namna bayana, vibaya sana au mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na haswa Viwango vyetu vya Jumuiya, tunaweza kusitisha au kulemaza kabisa uwezo wako kufikia akaunti yako. Tunaweza pia kusitisha au kulemaza akaunti yako ikiwa umekiuka mara kwa mara haki za mali miliki za watu wengine au pale tunapohitajika kufanya hivyo kwa sababu za kisheria. Pale ambapo tutachukua hatua kama hiyo, tutakufahamisha na kukueleza kuhusu chaguo zozote ulizo nazo kuomba ukaguzi mwingine, isipokuwa ikiwa kufanya hivyo kutatuweka au kuwaweka watu wengine kuwajibika kisheria; kuiumiza jumuiya ya watumiaji wetu, kutia doa au kuingilia maadili au uendeshaji wa vyanzo, mifumo au Bidhaa zetu zozote, ambapo tumewekewa vikwazo kutokana na vizuizi vya kiufundi; au pale ambapo tumewekewa marufuku ya kufanya hivyo kwa sababu za kisheria. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu kile unaweza kufanya iwapo akaunti yako imelemazwa na jinsi ya kuwasiliana nasi iwapo unafikiria tumelemaza akaunti yako kimakosa. Iwapo utafuta au tukilemaza akaunti yako, Masharti haya yatasitishwa kama makubaliano baina yako na sisi, lakini vipengele vifuatavyo vitaendelea kuhudumu: 3.3.1, 4.2-4.5. 3. Mipaka kwa dhima
Hakuna chochote katika Masharti haya kinacholenga kututenga au kuwekea mipaka kuwajibika kwetu kukitokea kifo, majeraha kwa mtu au uwakilishaji wa kuhadaa unaosababishwa na utepetevu wetu au kuathiri haki zako za kimaafikiano. Tutakutolea Bidhaa na huduma zetu kwa kuzingatia uadilifu kitaaluma na katika kudumisha mazingira salama na yasiyo na kosa. Alimradi tumezingatia uadilifu kitaaluma, hatutakubali kuwajibikia hasara ambazo hazijasababishwa na sisi kukiuka Masharti haya au vinginevyo matendo yetu; hasara ambazo wewe pamoja na sisi hatuwezi kutabiri wakati wa kuingia katika Masharti haya; na matukio ambayo hatuwezi kudhibiti. 4. Mizozo
Tunajaribu kutoa kanuni dhahiri ili tuweze kuweka mipaka au kwa matumaini kuzuia migogoro baina yako na sisi. Iwapo mzozo utatokea, hata hivyo, ni muhimu kufahamu mapema mahali inaweza kutatuliwa na sheria zitakazotumika. Iwapo wewe ni mtumiaji na kwa kawaida unaishi katika Muungano wa Umoja wa Ulaya, sheria za Taifa hilo zitatekelezwa kwenye dai lolote, hatua ya kuchukuliwa, au mgogoro ulio nao dhidi yetu unaotokana na au unaohusiana na Masharti haya au Bidhaa za Facebook ("dai"), na unaweza kutatua dai lako katika mahakama yoyote yenye uwezo katika nchi hiyo iliyo na mamlaka ya kuamua dai hilo. Katika hali nyingine zote, unakubali kuwa dai hilo lazima litatuliwe katika mahakama yenye uwezo katika Jamuhuri ya Ayalandi na kuwa sheria ya Kiirishi italinda Masharti haya na dai lolote, bila kuzingatia mgogoro wa utoaji wa sheria. 5. Nyingine
- Masharti haya (yaliyojulikana awali kama Taarifa ya Haki na Majukumu) yanaunda makubaliano kamili baina yako na Facebook Ireland Limited kuhusiana na matumizi yako ya Bidhaa zetu. Yanabadilisha makubaliano yoyote ya awali.
- Baadhi ya Bidhaa tunazotoa pia zinaongozwa kwa masharti ya ziada. Ikiwa unatumia Bidhaa yoyote kati ya hizi, utapewa nafasi ya kukubali masharti ya ziada ambayo yatakuwa sehemu ya makubaliano yetu nawe. Kwa mfano, iwapo utafikia au kutumia Bidhaa zetu kwa biashara au malengo ya kibiashara, kama vile kununua matangazo, kuuza bidhaa, kuendeleza programu, kudhibiti kikundi au Ukurasa kwa biashara yako, au kutumia huduma zetu za vipimo, lazima ukubaliane na Masharti yetu ya Biashara. Iwapo utachapisha au kushiriki maudhui yanayojumuisha muziki, lazima uzingatie Miongozo yetu ya Muziki. Kwa kiwango ambacho masharti yoyote ya ziada yanagongana na Masharti haya, masharti ya ziada yatatawala kiwango cha mgongano.
- Ikiwa sehemu yoyote ya Masharti haya itapatikana kuwa haiwezi kutekelezwa, sehemu zinazosalia zitaendelea kutumika kikamilifu. Tukishindwa kutekeleza sehemu yoyote ya Masharti haya, haitachukuliwa kama imeondolewa. Marekebisho au kuondolewa kwokote kwa Masharti haya lazima ufanywe katika maandishi na kuwekwa sahihi na sisi.
- Hutahamisha haki au majukumu yako yoyote chini ya Masharti haya kwa mtu mwingine bila kibali chetu.
- Unaweza kumteua mtu (anayejulikana kama mwasiliani wa kihistoria) kudhibiti akaunti yako iwapo imehifadhiwa kwenye kumbukumbu. Mwasiliani wako wa kihistoria pekee au mtu ambaye umemtambulisha kwenye wasia halali au waraka kama huo ukielezea wazi ridhaa ya kufichua maudhui yako unapofariki au kutoweza kuwajibika ataweza kutafuta ufichuzi kutoka kwenye akaunti yako baada ya kuhifadhiwa kwenye kumbukumbu.
- Masharti haya hayatoi haki zozote za wahusika wengine. Haki na majukumu yetu yote chini ya Masharti haya yanaweza kutolewa na sisi kwa urahisi kuhusiana na kuungana, umiliki, au mauzo ya mali, au kutumika kwa sheria au vinginevyo.
- Unapaswa kufahamu kwamba tunaweza kuhitaji kubadilisha jina la mtumiaji la akaunti yako katika hali fulani (kwa mfano, ikiwa mtu mwingine anadai jina hilo la mtumiaji na linaonekana kutohusiana na jina ambalo wewe hutumia kikawaida). Tutakufahamisha mapema ikiwa tutalazimika kufanya hivi na tutaeleza sababu za kufanya hivyo.
- Kila mara tunathamini majibu na mapendekezo yako mengine kuhusu bidhaa na huduma zetu. Lakini unafaa kujua kuwa tunaweza kuyatumia bila kizuizi au wajibu wowote wa kukufidia, na hatuna wajibu wa kuyaweka siri.
5. Masharti na sera nyingine zinazoweza kutekelezwa kwako
- Viwango vya Jumuiya: Miongozo hii inaelezea viwango vyetu kulingana na maudhui unayochapisha kwenye Facebook na shughuli yako kwenye Facebook na Bidhaa nyingine za Facebook.
- Masharti ya Biashara: Masharti haya yanatumika iwapo pia unafikia au kutumia Bidhaa zetu kwa lengo lolote la kibiashara, ikijumuisha utangazaji, kuendesha programu kwenye Jukwaa letu, kutumia huduma zetu za vipimo, kudhibiti kikundi au Ukurasa wa biashara, au kuuza bidhaa au huduma.
- Sera za Utangazaji: Sera hizi zinabainisha aina zipi za maudhui ya tangazo zinazoruhusiwa na washirika wanaotangaza katika Bidhaa za Facebook.
- Masharti ya Tangazo la Huduma Binafsi: Masharti haya yanatumika unapotumia violesura vya utangazaji wa huduma binafsi ili kuunda, kuwasilisha, au kupeleka tangazo au shughuli au maudhui mengine ya kibiashara au yaliyodhaminiwa.
- Sera ya Kurasa, Vikundi na Matukio: Miongozo hii inatumika iwapo utaunda au kusimamia Ukurasa wa Facebook, kikundi, au tukio au iwapo unatumia Facebook kuwasiliana au kusimamia tangazo.
- Sera ya Jukwaa la Facebook: Miongozo hii inaangazia sera ambazo zinatumika kwa matumizi yako ya Jukwaa letu (kwa mfano, kwa wasanidi programu au waendeshaji wa programu au tovuti ya Jukwaa au iwapo unatumia programu-jalizi za kijamii).
- Masharti ya Malipo ya Msanidi Programu: Masharti haya yanatumika kwa wasanidi programu wa programu zinazotumia Malipo ya Facebook.
- Masharti ya Malipo ya Jumuiya: Masharti haya yanatumika kwa malipo yote yanaiyolipwa kutumia Facebook.
- Sera za Biashara: Miongozo hii inaangazia sera zinazotumika unapotoa bidhaa na huduma za mauzo kwenye Facebook.
- Rasilimali za Chapa ya Facebook: Miongozo hii inaangazia sera ambazo zinatumika kwa matumizi ya alama za biashara, nembo na picha za skrini za Facebook.
- Miongozo ya Muziki: Miongozo hii inaangazia sera zinazotumika iwapo utachapisha au kushiriki maudhui yanayojumuisha muziki kwenye Facebook.
Tarehe ya Marekebisho ya Mwisho: Julai 31, 2019